Wachezaji wa Young Africana wakiwa mazoezini |
Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara timu ya Young
Africans leo imeendelea na mazoezi ya asubuhi katika viwanja vya hoteli
ya Sueno katika kuendelea kujiweka sawa kabla ya kuanza safari kesho
mchana ya kurejea nchini Tanzania tayari kwa mikikimikiki ya mzunguko wa
pili wa VPL 2013/2014.
Kocha mkuu Hans Van Der Plyum ameendelea kuwaandaa wachezaji wake na
kuyafanyia marekebisho kadhaa yaliyojitokeza katika mchezo uliopita
dhidi ya Simurq PIK kabla ya kesho kuanza safai ya kurejea nyumbani
tayari kwa kufungua dimba siku ya jumamosi dhidi ya Ashanti United.
Katika
mazoezi ya leo asubuhi kocha Hans amesema kikosi chake kinaendelea
vizuri mpaka sasa, hakuna majeruhi na wachezaji wanajituma na kuwajibika
kwa kujua wajibu wao ni nini hivyo inakua rahisi pia kushika maelekezo
yake.
Mara baada ya mazoezi ya asubuhi kocha Hans amesema timu
itaendelea tena na mazoezi ya jiioni kuanzia majira ya 9:30 kwa saa za
huku sawa na 10:30 kwa saa za Afrika Mashariki ambapo hayo ndo yatakua
mazoezi ya mwisho kabla ya kesho kuanza kwa safari ya kurejea Tanzania.
"Nina
uzoefu na soka la Afrika takribani kwa miaka 15, wachezaji niliowakuta
hapa Young Africans wana uwezo mzuri wote, wanajituma, wana nidhamu na
upendo wa hali ya juu kitu ambacho kwa mwalimu yoyote lazima atafurahia
mazingira hayo kwani hata ufanyaji wake kazi unakua mzuri "alisema
Hans."
Aidha Hans ameongeza kwa siku tisa alizokaa na wachezaji
wake Sueno Hotel Beach Side Antalya katika mazoezi na mafunzo aliyokuwa
anawapatia anaamini sasa timu yake ipo tayari kutetea Ubingwa wa Ligi
pamoja na kufanya vizuri kwenye na mashindano ya kimataifa .
Kambi
ya siku 14 katika hoteli ya Sueno Beach Side Manavgat jijini Antalya
imekua nzuri sana kwani wachezaji na benchi la ufundi kwa ujumla
wameweza kutimiza wajibu wao ambapo dhumuni kubwa ilikua ni kufanya
mazoezi, kupata michezo ya kirafiki kwa ajili ya maandalizi ya mzunguko
wa pili VPL na mashindano ya Klabu Bingwa barani Afrika.
Young
Africans ambayo imeweka kambi nchini Uturuki kwa takribani siku 14 mpaka
sasa, iliweza kucheza michezo minne ya kirafiki dhidi ya timu za Ankara
Sekerspor na Altay SK za Ligi Daraja la pili nchini Uturuki kabla ya
kuivaa timu ya KS Flumartari ya Albania kisha kumaliza na timu ya Simurq
PIK ya Azerbajain.
Matokeo ya mechi hizo ni:
11.01.2014
Young Africans 3 - 0 Ankara Sekerspor
(Didier 10, Okwi 46, Kiiza 61)
15.01.2014
Young Africans 2- 0 Altay SK
(Didier 46, Okwi 57)
18.01.2014
Young Africans 0 - 0 KS Flumartari
20.01.2014
Young Africans 2 - 2 Simurq PIK
(Didier 13, Ngasa 30) - (Anderson 45, Sattarli 56)
No comments:
Post a Comment