KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Tuesday, January 21, 2014

Paul Ince afukuzwa kazi Blackpool

Kiungo wa zamani wa England Paul Ince amefutwa kazi na klabu ya Blackpool hiyo jana.
Ince amefukuzwa na klabu hiyo kutoka pande za Kaskazini-Magharibi mwa England kufuatia kikosi hicho kuchapwa michezo tisa kati ya kumi ya hivi karibuni ambapo Blackpool imeweza kuambulia alama moja katika ligi ndogo ya 'English football's Championship' likiwa ni daraja dogo la chini ya 'Premier League' tangu mwezi Novemba.
Sambamba naye waliofukuzwa kutoka Bloomfield Road ni wasaidizi wake wawili Alex Rae na Steve Thompson.
Klabu hiyo imesema kwasasa mkongwe wa klabu hiyo kiungo wa zamani Barry Ferguson mwenye umri wa miaka 35 atasimamia mazoezi ya kikosi hicho kuanzia alhamisi.

No comments:

Post a Comment