Kombe la League Cup limeibuka kama nafasi ya mwisho ya mabingwa wa
ligi ya Premier ya Uingereza, Manchester United, kuokoa msimu ambao
unazidi kukumbwa na huzuni kila kuchao.
Huku uteteaji wa taji lao la ligi kuu ukisambaratika baada ya kuchakazwa 3-1
ugenini na Chelsea Jumapili na kuwaacha alama 14 nyuma ya viongozi, magwiji
hao pia waling'olewa kutoka kombe la FA kwa kuabishwa 2-1 na Swansea.
Ingawa michuano ya kombe la League Cup lilipuuziwa mara kwa mara na
mtangulizi wa meneja, David Moyes, Sir Alex Ferguson, meneja huyo wa sasa hana budi kutumia viungo wake mahiri watakapo waalika Sunderland Old
Trafford Jumatano.
United wana kibarua cha kupindua matokeo ya kichapo cha mabao 2-1 katika awamu ya
kwanza ya nusu-fainali yao uwanja wa Stadium of Light.
“Tutafanya lolote ili kufuzu ili kuwapa mashabiki jambo la
kusherehekea. Kumetokea masaibu mengi na ninafahamu hayo kikamilifu,”
Moyes aliambia runinga ya klabu hicho, MUTV.
Meneja huyo ambaye amejiweka katika shinikizo baada ya kudorora kimatokeo katika kampeni hii ameshuhudia timu hiyo ikipoteza mechi nne kati
ya tano tangu Januari 7.
Kiungo wake, Michael Carrick, amesema United hawana lingine ila kutafuta suluhu ya dharura kurejelea ushindi.
“Tuna hamu ya kurejea tena haraka iwezekanyavyo. Jumatano tuna
kibarua kikubwa kwani ni nafasi ya kufuzu fainali ya michuano na
hatupuuzii. Tutajiinua kutoka kupoteza katika mchezo dhidi ya Chelsea na tuko tayari
kupambana Jumatano,” Carrick alisema.
No comments:
Post a Comment