Nigeria iliziangamiza kabisa ndoto za wenyeji Afrika Kusini za kusonga
mbele kutoka awamu ya makundi ya dimba la kombe la mataifa ya Afrika kwa
wachezaji wa ndani - CHAN, baada ya kuwalaza magoli matatu kwa moja.
Ushindi huo sasa una maana kuwa The Super Eagles wanajiunga na washindi
wa kundi A, Mali katika awamu ya robo fainali. Mali iliizaba Msumbiji
magoli mawili kwa moja. Katika mechi za Jumamosi, Burundi ilichukua
usukani wa kundi D baada ya kuizidi nguvu Mauritania kwa kuifunga magoli
matatu kwa mawili.
Burundi wanaongoza kundi hilo na pointi nne wakati Gabon wakiwa wa pili
na pointi nne pia baada ya kuwafunga Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo
goli moja kwa sifuri. Kongo ina pointi tatu. Mechi za mwisho za kundi
hilo zinachezwa Jumatano wakati Mauritania wakipambana na Gabon, huku
nao viongozi Burundi wakishuka dimbani na Jamhuri ya Kidemokrasia ya
Kongo.
Uganda inaongoza kundi B na pointi nne ikifuatia na Morocco na Zimbabwe
ambazo zina piinti mbili kila mmoja, nayo Burkina Faso ikiwa na pointi
moja. Katika Kundi C, viongozi ni Libya na Ghana ambazo zina pointi nne,
Kongo Brazaville katika nafasi ya tatu na pointi tatu, nayo Ethiopia
ikishika mkia bila pointi yoyote.
No comments:
Post a Comment