Katika ligi kuu ya Premeir nchini England, Pepe Mel
alianza kampeini yake kama meneja wa Westbrom kwa kuzoa alama moja pale
timu yake ilipotoka sare ya kufungana bao moja kwa moja na Everton.
Kufuatia sare hiyo Everton imesalia katika
nafasi ya tano na alama 42 ili hali Westron pia ikasalia katika nafasi
yake ya kumi na mbili.
Kevin
Mirallas alifungia bao na kuiweka Everton uongozini katika kipindi cha
kwanza kabla ya Lugano kusawazisha dakika kumi na tano kabla ya mechi
hiyo kumalizika.
Huku kocha huyo mpya akifurahia matokeo yake kocha wa Everton, Roberto Martinez amegadhabishwa na matokeo hayo.
Martinez amesema wachezaji wake walipoteza
nafasi nyingi za kufunga katika kipindi cha kwanza na kuwa kiwango chao
kilishuka sana katika kipindi cha pili.
Wakati huo huo, wasimamizi wa mtandano wa
Zoopla, wametangaza kuwa wamesitisha ufadhili wao kwa klabu ya Westbrom,
kufuatia mzozo unaohusiana na madai ishara ya ubaguzi dhidi ya
wayahudi, iliofanywa na mshambulizi wake Nicolas Anelka.
Anelka alionyesha ishara hiyo baada ya kufunga bao wiki tatu zilizopita.
Wanaharakati wa kupinga ubaguzi wa rangi na
makundi ya kiyahudi wanasema wanataka mchezaji huyo kupigwa marufuku,
lakini klabu hiyo imekariri kuwa Anelka ana haki ya kuendelea kucheza.
Mel alimjumuisha Anelka katika kikosi chake
kilichochuana na Everton, huku shirikisho la mchezo wa soka FA
likiendelea na uchunguzi wake kuhusiana na sakata hiyo.
No comments:
Post a Comment