KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Tuesday, January 21, 2014

Mgombea Urais wa FIFA aanza kampeni kwa kuahidi mageuzi makubwa

Aliyekuwa naibu katibu mkuu wa FIFA Jerome Champagne ametangaza nia yake ya kugombea kiti cha urais wa FIFA kuchukua nafasi ya Sepp Blatter. Champagne mwenye umri wa miaka 55 atawania katika uchaguzi wa 2015.
 Blatter aliiambia televisheni moja ya Ufaransa wiki iliyopita kuwa atatangaza kama atagombea tena uchaguzi wa rais au la, kabla ya mkutano mkuu wa FIFA mjini Sao Paolo mnamo Juni 10 na 11. Blatter mwenye umri wa miaka 77 amekuwa katika wadhifa huo tangu mwaka wa 1998.
Rais wa sasa wa Shirikisho la Soka barani Ulaya – UEFA, Michel Platini alisema mwaka jana kuwa atatangaza kama atagombea wadhifa wa urais wa FIFA au la, wakati wa Kombe la Dunia nchini Brazil au baada ya tamasha hilo ambalo linang'oa nanga Juni 12 hadi Julai 13.
Rousseff kukutana na Blatter
Huku ikiwa imesalia chini ya miezi mitano tu tukielekea nchini Brazil kwa dimba la Kombe la Dunia, Rais wa Brazil Dilma Rousseff atakutana na Rais wa Shirikisho la Soka Duniani – FIFA Sepp Blatter pembezoni mwa Jukwaa la Kimataifa la Kiuchumi mjini Davos litakaloandaliwa wiki ijayo, ili kujadili kuhusu maandalizi ya tamasha hilo la soka ulimwenguni.
Viongozi hao wawili watakutana baada ya Blatter kuikosoa Brazil mapama mwezi huu kwa kujikokota katika maandalizi ya fainali za kombe la dunia, ikilinganishwa na mataifa mengine yaliyowahi kuandaa dimba hilo, katika kipindi cha miaka 16 ya uongozi wake. Aliwashutumu waandilizi wa Brazil kwa kuanza maandalizi wakiwa wamechelewa baada ya kupewa kibali cha kuwa mwenyeji wa kinyang'anyiro hicho mnamo mwaka wa 2007. Viwanja 6 kati ya 12 vitakavyotumiwa, havijatimiza muda wa mwisho uliowekwa na FIFA wa Desemba 31.
Jerome Champagne, amependekeza kuanzishwa kwa mfumo wa kutoa kadi ya chungwa wakati wa mechi za soka, ili kuruhusu marefa wa mechi kuwaruhusu wachezaji waliofanya madhambi kuondolewa uwanjani kwa muda.
Champagne mwenye umri wa miaka hamsini na tano kutoka Ufaransa, aliyasema hayo siku ya Jumatatu wakati alipoanzisha kampeini yake ya kumrithi Sepp Blatter kama rais wa FIFA.
Amesema ikiwa atashinda atapendekeza vilabu vya soka kuadhibiwa ikiwa wachezaji wake watahoji maamuzi ya refa na vile vile kuchunguza uwezekano wa kutumia teknolojia kutatua maamuzi muhimu.
Uchaguzi wa urais wa FIFA utafanyika mjini Zurich Juni mwaka wa 2015.
Miongoni mwa mapendekezo mengine aliyoyasema ni kuthibiti idadi ya wachezaji wa kigeni wanaosajiliwa na vilabu, kutangazwa kwa mshahara wa rais wa FIFA na maafisa wengine wakuu.
Aidha ameahidi kuwa atafutilia mbali sheria ya sasa inayotoa adhabu tatu kwa mchezaji ambaye atafanya madhambi katika eneo la hatari.
Kuambatana na sheria ya sasa mchezaji yeyote anayefanya kosa katika eneo la hatari, hupewa kadi nyekundi moja kwa moja na pia kupigwa marufuku ya kutocheza mechi mbili zinazofuata.

No comments:

Post a Comment