KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Friday, January 3, 2014

Rashid Gumbo, Semmy Kessy na Salum Kinje waombewa ITC na La Passe ya Ushelisheli

Nyota wa Zamani wa Simba, Yanga na Mtibwa Sugar Rashidi Gumbo
Shirikisho la Mpira wa Miguu la Shelisheli (SFF) limetuma Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) maombi ya Hati ya Uhamisho ya Kimataifa (ITC) kwa wachezaji watatu wa Tanzania.


Wachezaji walioombewa hati hiyo ili wakajiunge na timu ya La Passe FC inayocheza Ligi Kuu nchini humo ni Salum Kinje aliyekuwa akiichezea timu ya Simba, Semmy Kessy aliyekuwa Lipuli ya Iringa na Rashid Gumbo aliyekuwa timu ya Mtibwa Sugar.


TFF inafanyia kazi maombi hayo na mara taratibu zitakapokamilika hati hizo zitatolewa.

No comments:

Post a Comment