KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Thursday, February 20, 2014

Nahodha wa Man Utd Nemanja Vidic amekaribia kwa asilimia 90 kukamilisha mpango wa kujiunga na Inter Milan

Rais wa Inter Milan Erick Thohir anasema wanakaribia kukamilisha mpango wa kumsjili nahodha wa Manchester United Nemanja Vidic.
Mlinzi huyo wa zamani wa Serbia ambaye kwasasa ana umri wa miaka r, 32, atakuwa mchezaji huru kufikia kumalizika kwa msimu huku klabu hiyo ya nchini Italia ikiwa imekamia kupata saini yake

Vidic akiwa na Man Utd

Manchester United's Nemanja Vidic with the Premier League trophy at Old Trafford in 2011
  • Dec 25 2005: Alikubali kujiunga na United akitokea Spartak Moscow ya Russia
  • Jan 25 2006: Alianza kuicheza United katika mchezo dhidi ya Blackburn
  • Premier League titles: 2007, 2008, 2009, 2011, 2013
  • Champions League: 2008
  • League Cup: 2006, 2009, 2010
Thohir ameuambia mtandao wa Inter Milan kuwa 
"Sitaki kutangaza kitu ambacho kimefikia hatua ya asimilia 90% nafikiri ni bora kutangaza lini zoezi hilo litakamilika.
 "Sitaki kusemea kitu ambacho bado hakija kamilika bado"

Vidic ambaye amekuwa na Manchester United tangu 2006 baada ya kuhamia kwa ada ya pauni milioni £7 akitokea Spartak Moscow, alithibtisha mapema mwezi huu kuwa ataelekea kucheza soka nje ya England mara baada ya mkataba wake na United ukatakapo malizika kiangazi.

Alisema hayo Februari 7 na kunukuliwa 
 "Nimeamua kuwa nitaondoka mwishioni mwa msimu. Nataka kujipa changamoto tena na najaribu kusaka ubora tena katika miaka ijayo"
Inter iko katika nafasi ya tano katika ligi kuu ya Italia Serie A, alama 11 nyuma ya timu iliyo katika nafasi ya tatu Napoli, ambao wanakamata nafasi ya mwisho ya ufaulu wa kucheza michuano ijayo ya Champions League.
Inter inayonolewa na Walter Mazzarri, inapigana kuimarisha safu yake ya ulinzi kutokana na kuruhusu magoli mengi katika ligi msimu huu kuliko timu nyingine yoyote katika ligi hiyo zilizo katika nafasi sita za juu.

No comments:

Post a Comment