KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Thursday, March 20, 2014

George Boyd wa Hull City asimamishwa michezo mitatu kwa kumtupia maneno machafu Joe Hart wa City

Winga wa Hull City George Boyd atakuwa akitumikia kibano cha kukosekana kwa michezo mitatu baada ya chama cha soka nchini England FA kujiridhisha kuwa alimtolea maneno ya kadhia mlinda mlango Joe Hart .

Winga huyo mwenye umri wa miaka 28 alimfanyia mlinda mlango huyo wa Manchester City wakati wa mchezo wa Jumamosi iliyopita mchezo wa ligi ya England katika dimba la KC Stadium, mchezo ambao wageni City waliibuka na ushindi wa mabao 2-0.

Tukio hilo lililotokea dakika ya 68, halikuwezakushuhudiwa na mwamuzi Lee Mason aliyechezesha pambano hilo wala wasiadizi wake lilionekana baadaye kwa njia ya video na FA kujiridhisha.
Boyd alikanusha kutenda kosa hilo lakini hata hivyo rufaa yake ilikataliwa na jopo la wajumbe watatu waliosikiliza shauri hilo.

Hart alionyeshwa kadi ya njano kwa kughasi Boyd kufuatia winga huyo kudondoka baada ya kukabiliana katika eneo la hatari. 

Mlinda mlango huyo namba moja wa England number anaamini kuwa winga huyo alijirusha yaani 'dived', na kuanza kumsukuma kabla ya kuanza kutupiana maneno machafu kila mmoja.

No comments:

Post a Comment