KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Monday, March 17, 2014

Masikini David Moyes akiri kuwa kibarua cha kuiongoza Man United ni kigumu

Hatimaye meneja wa Manchester United, David Moyes, amekiri kuongoza miamba hao wa Uingereza ni kibarua kigumu kuliko vile alitarajia.
Taarifa hiyo inatia shaka kubwa kuwa meneja huyo aliyetoka Everton hana uwezo wa kumudu hadhi ya kuwaongoza mabingwa hao mara 20 wa taji la ligi ya Uingereza.
Akizungumuza baada ya kupoteza mechi yake ya tano nyumbani katika Premier musimu huu mikononi mwa waasimu wao wa jadi, Liverpool, Moyes alikubali kwamba kibarua cha United kimekuwa changamoto ambayo hakukisia.

“Kazi ikikuwa ngumu kutoka mwanzo. Lakini imekuwa ngumu zaidi ya nilivyotarajia,” Moyes alikiri.

“Hilo linaonyesha kuwa hatupati matokeo yanayostahili. Ni lazima tucheze vyema zaidi ili iwe ni vigumu kututawala huku tukihakikisha ya kwamba tunabuni nafasi na kufunga mabao zaidi.”
United wanadorora katika nafasi ya saba, alama 18 nyuma ya vingozi Chelsea baada ya kushinda ligi hiyo na mwanya wa pointi 11 musimu jana.

No comments:

Post a Comment