KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Saturday, March 15, 2014

Wachezaji 40 wa maboresho ya timu ya taifa ya wang'amuzi wa vipaji kutangazwa Jumatatu

Mchakato wa ung’amuzi wa vipaji kwa ajili ya maboresho ya Taifa Stars ulioshirikisha wang’amuzi wa vipaji (scouts) zaidi ya 40 umekamilika leo (Machi 15 mwaka huu) na majina ya wachezaji yatatangazwa Jumatatu (Machi 17 mwaka huu)

Wachezaji hao watafanyiwa vipimo vya afya (medical check up), kabla ya kuingia kambini Tukuyu mkoani Mbeya. Wachezaji watakaoingia kambini ni wale watakaokuwa wamefaulu vipimo.

Wang’amuzi vipaji waliokuwa Lushoto ni Abdul Mingange, Ayoub Nyenzi, Boniface Pawasa, Charles Mkwassa, Dan Korosso, Dk. Mshindo Msolla, Edward Hiza, Elly Mzozo, Hafidh Badru, Hamimu Mawazo, John Simkoko, Jonas Tiboroha, Juma Mgunda na Juma Mwambusi.

Kanali mstaafu Idd Kipingu, Kenny Mwaisabula, Kidao Wilfred, Madaraka Bendera, Madaraka Selemani, Mbarouk Nyenga, Mohamed Ally, Mussa Kissoky, Nicholas Mihayo, Pelegrinius Rutayuga, Peter Mhina, Salum Mayanga, Salvatory Edward, Salum Madadi, Sebastian Nkoma, Sekilojo Chambua, Selemani Jabir na Shabani Ramadhan.

Wengine ni Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ufundi, Kidao Wilfred, Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Vijana, Ayoub Nyenzi, Kaimu Mkurugenzi wa Ufundi, Salum Madadi na Mshauri wa Rais (Ufundi), Pelegrinius Rutayuga.

No comments:

Post a Comment