22/04/2014
YAH:
MASHINDANO YA 16 YA MPIRA WA KIKAPU (BASKETBALL)
KWA
MAJIJI YA AFRIKA KANDA YA TANO
(EAST
CENTRAL & AFRICA INTERCITY BASKETBALL GAMES)
Mashindano
ya 16 ya Mpira wa Kikapu kwa Majiji ya Afrika Kanda ya Tano na Majiji
alikwa kutoka Kanda zingine za Afrika yanatarajiwa kufanyika Jijini
Dar es Salaam, Tanzania.
Mashindano
yatafanyika:-
Mwezi
wa Tano (May)
Tarehe
6 hadi 11
Mwaka
2014
Majiji
yanayotarajiwa kushiriki ni Dar es Salaam (wenyeji), Mwanza, Mbeya,
Arusha na Tanga kutoka Tanzania.
Nairobi,
Mombasa na Kisumu kutoka Kenya.
Kampala
na Mukomo kutoka Uganda.
Bujumbura
– Burundi na Kigali-Rwanda.
Mogadishu
na Hargeisa kutoka Somalia.
Juba
na Citizen kutoka Sudani ya Kusini.
Adis
Ababa – Ethiopia na Cairo-Misri.
Mashindano
ya 15 ya Majiji yalifanyika mwezi May mwaka jana (2013) jijini
Kampala; ambapo Jiji la Mukono nchini Uganda lilitwaa ubingwa kwa
wanaume na Nairobi walitwaa ubingwa kwa wanawake.
Ni
matarajio ya Kamati ya uendeshaji ya Majiji (Intercity Coordinating
Committee) na Bodi ya Intercity, kwamba Majiji yote matano ya
Tanzania yatakuwa yanajiandaa vyema ili kushiriki na kuhakikisha kuwa
ubingwa unabakia Tanzania.
Tunatoa
wito kwa utawala wa Jiji la Dar es Salaam kushirikiana na uongozi wa
Chama cha Mpira wa Kikapu Mkoa wa Dar es Salaam ili kuitumia fursa
hii kulitangaza Jiji na kuwapatia wafanya biashara nafasi ya kuongeza
uchumi wao. Pia Halmashauri zote tatu za Ilala, Temeke na Kinondoni
kushiriki katika kuziandaa timu za wanawake na wanaume za Jiji la Dar
es Salaam kwa kiwango cha kutwaa ubingwa.
Ingefaa
nafasi ya kwanza ya udhamini ichukuliwe na Jiji pamoja na Halmashauri
zake tatu za Ilala, Temeke na Kinondoni na kwa pamoja kuwaalika
wafanyabiashara wa Jiji la Dar es Salaam kuwaunga mkono ili shindano
liwe zuri na lenye mafanikio makubwa.
Tunatoa
wito kwa Utawala wa Majiji ya Arusha, Mbeya, Mwanza na Tanga kusaidia
maandalizi ya timu zao kwa kushiriki moja kwa moja na kwa kushawishi
wadhamini wengine kudhamini timu za majiji yao.
Imetolewa
na kamati ya uendeshaji ya Majiji ya Africa Kanda ya Tano, Mchezo wa
Mpira wa Kikiapu.
Mbaga
Mwamboma
Katibu,
Bodi ya wakurugenzi.
No comments:
Post a Comment