KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Tuesday, April 22, 2014

VIINGILIO MECHI YA STARS, BURUNDI VYATAJWA

Kiingilio cha chini katika mechi ya kirafiki ya kimataifa kati ya timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) na Burundi (Intamba Mu Rugamba) itakayochezwa Aprili 26 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam ni sh. 5,000.

Mechi hiyo itakuwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 50 ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar, na kiingilio hicho ni kwa viti vya rangi ya chungwa, bluu na kijani. Kwa wa VIP A kiingilio kitakuwa sh. 20,000 wakati VIP B na C ni sh. 10,000.

Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager tayari ipo kambini kwenye hoteli ya Kunduchi Beach kujiandaa kwa ajili ya mechi hiyo itakayochezeshwa na waamuzi kutoka nchini Kenya.

Burundi inatarajia kuwasili nchini keshokutwa (Aprili 22 mwaka huu) tayari kwa ajili ya mechi hiyo inayotajiwa kuwa ya kusisimua. Mechi hiyo imepangwa kuanza saa 10 jioni.

Wachezaji wa Taifa Stars waliopo kambini ni Deogratias Munishi, Mwadili Ali, Aidan Michael, Aggrey Morris, Erasto Nyoni, Hassan Mwasapili, Kelvin Yondani, Said Moradi, Amri Kiemba, Frank Domayo, Himid Mao, Jonas Mkude, Athanas Mdamu, Haruna Chanongo, Juma Liuzio, Khamis Mcha, Mrisho Ngasa, Ramadhan Singano na Simon Msuva.

Wengine ni Benedicto Mlekwa, Emma Simwanda, Joram Mgeveje, Omari Kindamba, Edward Mayunga, Shiraz Sozigwa, Yusuf Mlipili, Said Ally, Abubakar Mohamed, Hashim Magona, Omari Nyenje, Chunga Zito, Mohammed Saidi, Ayoub Lipati, Abdurahman Ally na Paul Bundara.

BONIFACE WAMBURA
OFISA HABARI NA MAWASILIANO
SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)

No comments:

Post a Comment