KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Saturday, April 19, 2014

UTEUZI TIMU YA TAIFA: Salum Abubakar 'sureboy' na Ivo Mapunda waachwa huku Shomari Kapombe akiendelea kusalia nje kufuatia kuikimbia AS Cannes ya Ufaransa

Walinda mlango wa Azam fc Aishi Manula na Mwadini Ally wote waitwa Taifa Stars
KOCHA Msaidizi wa Taifa Stars, Salum Mayanga amewachukua makipa wote wa mabingwa wapya wa Bara, Azam FC Mwadini Ally na Aishi Manula katika kikosi chake cha wachezaji wengine 23 watakaoingia kambini kesho (Aprili 20 mwaka huu) kuungana na 16 waliotajwa awali kujiandaa kwa mechi ya kirafiki dhidi ya Burundi itakayochezwa Aprili 26 mwaka huu.
 
Kwa ujumla, Mayanga amechukua wachezaji saba wa Azam FC wengine ni mabeki Aggrey Morris, Erasto Nyoni na Said Moradi na viungo Himid Mao na Khamis Mcha.
 
Hata hivyo uteuzi huo umemuweka kando mlinda mlango mzoefu wa Simba Ivo Mapunda ambaye katika siku za hivi karibuni mlinda mlango huyo amekuwa akijumuishwa katika kikosi hicho baada ya kiwango chake kupanda kwa wakati akiichezea klabu bingwa ya kenya AFC Leopards ya Kenya kabla ya kung'ara zaidi katika michuano ya Chalenji iliyofanyika nchini Kenya.
 
Pia kikosi hicho kinaendelea kumkosa mlinzi mahiri Shomari Kapombe kuelekea kwenye mchezo maalum wa kusheherekea sikukuu ya muungano ambapo Taifa stars itakuwa ikicheza dhidi ya timu ya taifa ya Burundi 'Intamba Murugamba' mchezo ambao umepangwa kufanyika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam tarehe 26/04/2014.

Kapombe ambaye kimsingi ni mchezaji halali wa timu ya daraja la nne ya AS Cannes ya nchini Ufaransa, alirudi Tanzania Novemba mwaka jana kuichezea timu ya taifa 'Taifa Stars' dhidi ya Zimbabwe kwenye mechi ya kirafiki,na  tangu hapo amegoma kurudi Ufaransa kwa madai kuwa hajapewa mshahara kwa muda wa miezi mitatu.
 
Kuwepo kwake nchini kumemfanya mchezaji huyo kukosa sifa ya kuichezea timu ya taifa huku taarifa zikisema kuwa vilabu vya Azam fc, Yanga na Simba vikipambana kumvisha jezi zao msimu ujao wa ligi ya Tanzania Bara licha ya Azam fc tayari wakionekana kuwahi kufanya hivyo.
 
Wachezaji wengine wazoefu ambao wamekosa nafasi kikosini ni pamoja na nahodha wa Yanga Nadir Ally Horoub' Kanavaro' Salum Abubakar 'Sureboy' na mlinda mlango Juma Kaseja.   
 
Kikosi kamili cha Stars ni makipa; Aishi Manula (Azam FC), Mwadini Ally (Azam FC) na Deogratias Munishi (Yanga SC). 
 
Mabeki Abdi Banda (Coastal Union), Aidan Michael (Ruvu Shooting), Aggrey Morris (Azam FC), Erasto Nyoni (Azam FC), Hassan Mwasapili (Mbeya City), Kelvin Yondani na Said Moradi (Azam FC).
 
Viungo; Amri Kiemba (Simba SC), Frank Domayo (Yanga SC), Himid Mao (Azam FC) na Jonas Mkude (Simba SC). 
 
Washambuliaji; Athanas Mdamu (Alliance), Haruna Chanongo (Simba SC), Juma Liuzio (Mtibwa Sugar), Khamis Mcha (Azam FC), Mbwana Samata (TP Mazembe, DRC), Mrisho Ngassa (Yanga SC), Mwinyi Kazimoto (Markhiya, Qatar), Ramadhan Singano (Simba SC), Simon Msuva (Yanga SC) na Thomas Ulimwengu (TP Mazembe, DRC).
 
Wachezaji walioitwa kutoka katika kikosi cha maboresho ni kipa Benedicto Tinoko Mlekwa (Mara), mabeki wa kati; Emma Namwondo Simwanda (Temeke) na Joram Nason Mgeveje (Iringa). 
 
Walinzi wa pembeni ni Omari Ally Kindamba (Temeke), Edward Peter Mayunga (Kaskazini Pemba) na Shiraz Abdallah Sozigwa (Ilala).
 
Viungo ni Yusuf Suleiman Mlipili (Temeke), Said Juma Ally (Mjini Magharibi), Abubakar Ally Mohamed (Kusini Unguja), Hashim Ramadhan Magona (Shinyanga), Omari Athumani Nyenje (Mtwara) na Chunga Said Zito (Manyara).
 
Washambuliaji ni Mohammed Seif Saidi (Kusini Pemba), Ayoub Kasim Lipati (Ilala), Abdurahman Othman Ally (Mjini Magharibi), Paul Michael Bundara (Ilala). Wachezaji wa U 20 ni Mbwana Mshindo Musa (Tanga) na Bayaga Athanas Fabian (Mbeya). Taifa Stars  itaingia kambini kwenye hoteli ya Kunduchi Beach.

No comments:

Post a Comment