Katibu Mkuu wa Yanga SC, Beno Njovu (kushoto) akiongea na wandishi wa habari, kulia ni aliyekua kocha mkuu wa Yanga Hans Van der Pluim |
Hans Van Der Pluijm kocha mkuu wa
timu ya Young Africans leo amewaaga rasmi wachezaji wake, viongozi,
wapenzi na wanachama baada ya kumalizaa wake wa miezi sita na sasa
anakwenda kujiunga na timu Al Shoalah FC iliyopo Ligi Kuu nchini Saudi
Arabia.
Kocha huyo mdachi ambaye ameiongoza Young Africans kwa kipindi cha
miezi mitano amesema anashukuru kwa sapoti aliyokua akiipata kutoka kwa
wachezaji, viongozi, wapenzi na wanachama wa timu hii kwa kipindi chote
alipokuwa nchini Tanzania.
"Najua wengi itawashangaza kuona
naondoka lakini ukweli ni kwamba nilikuwa na hiyo deal hata kabla ya
kuja Yanga, nilikuwa na makubaliano na timu ya Al Shoalah FC makubaliano
ambayo yanaanza mwezi ujao hivyo nilikubaliana na viongozi wa Yanga kuja
kufanya kazi kwa kipindi cha miezi sita tu, nashukuru tumefanya kazi
salama na baada ya mkataba huo kuisha nipo tayari kurudi kuja kufanya
kazi Tanzania" alisema Hans
Naipenda Yanga SC, nimejaza fomu
kuomba uanachama hivyo mimi ni sehemu ya Yanga na katika usajili ujao
nitawasaidia kuleta wachezaji wazuri ambao wataisaidia timu kwenye msimu
ujao kwa Ligi ya Vodacom na mashindao ya Kimataifa.
Kocha Hans
anaondoka leo na kwenda Ghana kisha baadae atakwenda nchini Saudu Arabia
tayari kwa kujiandaa na maandalizi ya msimu ujao katika timu yangu hiyo
ambayo nitaitumikia kwa kipindi cha mwaka mmoja.
Kuhusu usajili kocha mkuu ameshakabidhi ripoti yake ya kiufundi jana, viongozi wanaifanyia kazi kisha baadae itawekwa wazi.
No comments:
Post a Comment