Makamu Mwenyekiti wa kalbu ya Yanga SC Bw Clement Sanga (katikati) akiongea na waandishi wa habari makao makuu ya Benki ya Posta, kulia ni mkurugenzi masoko wa Benki ya Posta Bw. Deo Kwiyukwa |
Klabu ya Young Africans imeeingia makubaliano na Benki ya Posta
nchini juu ya mabadiliko ya utengenezaji wa kadi za wanachama kutoka
kwenye mfumo wa zamani (analogy) kwenda kwenye mfumo mpya wa kisasa
(digital) ambapo sasa wanachama wake watakua wakitumia kadi zenye mfumo
wa ATM.
Mkurugenzi Masoko wa Benki ya Posta nchini Bw. Deo
Kwiyukwa amesema wamefikia makubaliano hayo baada ya kukaa na viongozi
na kuona njia hiyo itaisaidia klabu kuongeza mapatao kwani wigo wake wa
kuandikisha wanachama utakua ni mkubwa kwa nchi nzima na kwa muda mfupi.
"Badala
ya wanachama kuja Dar es salaam makao makuu kujaza fomu za uanachama
watakua wanaweza kufanya hivyo popote walipo kwa kwenda ofisi za Benki
ya Posta na kujaza fomu hizo na baadae kupewa kadi ya uanachama" alisema
Deo.
Gharama za kujiunga na uanchama
zitabakia zile zile Tshs 15,000/=, na ada ya mwaka elfu Tshs 12,000/=
ambapo mwanachama wa Yanga atapata kadi ya TPB yenye logo ya timu yake
ambayo pia ataitumia kwenye shughuli za kibenkI kwa huduma ya kuweka na
kutoa fedha.
Naye Makaumu Mwenyekiti wa Klabu
ya Yanga Clement Sanga amesema anaishukuru Benki ya Posta kwa kuweza
kufikia makubalianao hayo, kwa kutumia mfumo huu wa kisasa tutaweza
kujua idadi ya wachama wetu walio hai kwa wepesi zaidi na taarifa zetu
zitaweza kuwafikia wanachama kwa uharaka zaidi.
Uzinduzi
rasmi wa kadi mpaya za uanachama utafanyika tarehe 16.05.2014 kwenye
hoteli ya Hyatt Kempsinki eneo la Posta (zamani Kilimanjaro Hotel) na
mara baada ya uzinduzi moja kwa moja zoezi la kuhamisha wanachama kutoka
kwenye mfumo wa analogy kwenda digital utaanza.
No comments:
Post a Comment