Uwanja wa kumbukumbu ya Waziri mkuu wa zamani nchini Tanzania marehemu Edward Moringe Sokoine uliopo jijini Mbeya |
Michuano ya Ligi ya Mabingwa wa Mikoa (RCL)
inayoshirikisha timu 27 inaanza kutimua vumbi kesho (Mei 10 mwaka huu) katika
vituo vitatu vya Morogoro, Mbeya na Shinyanga kwa mechi mbili kila siku.
Kundi A
ambalo mechi zake zinachezwa Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro, African Sports
ya Tanga itacheza na Kiluvya United FC ya Pwani saa 8 mchana wakati saa 10
jioni ni Mji Mkuu FC (CDA) ya Dodoma dhidi ya Pachoto Shooting Stars ya Mtwara.
Jumapili
(Mei 11 mwaka huu) katika kundi hilo kutakuwa na mechi kati ya Bulyanhulu FC
(Shinyanga) na Kariakoo SC (Lindi) itakayoanza saa 8 mchana wakati saa 10 jioni
ni Navy FC (Dar es Salaam) na Abajalo FC pia ya Dar es Salaam.
Kundi B
katika Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya litaanza ligi kwa mechi
kati ya Ujenzi (Rukwa) na Volcano FC (Morogoro) saa 8 mchana wakati saa 10
jioni ni AFC ya Arusha na Panone FC ya Kilimanjaro.
Mei 11
mwaka huu saa 8 mchana ni Mpanda United ya Katavi na Magereza ya Iringa wakati
Tanzanite (Manyara) na Njombe Mji (Njombe) zenyewe zitaumana kuanzia saa 10
jioni.
Simiyu
United ya Simiyu na Mvuvumwa FC (Kigoma) ndizo zitakazoanza kucheza saa 8 mchana
katika kundi C linalotumia Uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga. Saa 10 jioni ni
mechi kati ya Wenda FC ya Mbeya na mabingwa wa Mkoa wa Kagera, Eleven Stars FC.
Jumapili
(Mei 11 mwaka huu), mechi za kundi hilo zitakuwa Singida United (Singida) na
Mbao FC ya Mwanza kuanzia saa 8 mchana wakati jioni ni pambano kati ya mabingwa
wa Mkoa wa Mara, JKT Rwamkoma FC na Geita Veterans FC ya Geita.
Ligi
hiyo itamalizika Juni 2 mwaka huu ambapo timu itakayoongoza kila kundi itapanda
daraja kucheza Ligi Daraja la Kwanza (FDL) msimu wa 2014/2015.
Uwanja wa Jamhuri mkoani Morogoro wakati ulipokuwa katika ukarabati hivi karibuni |
No comments:
Post a Comment