Makocha
wa timu za Tanzania (Ngorongoro Heroes), John Simkoko na Nigeria (Flying
Eagles), Manu Garba wanakutana na waandishi wa habari kuzungumzia mikakati yao kwa
ajili ya mechi ya Jumapili.
Mkutano
huo utafanyika kesho (Mei 10 mwaka huu) kwenye ukumbi wa mikutano wa Shirikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kuanzia saa 5 kamili asubuhi.
Mechi
hiyo ya kwanza ya raundi ya pili ya michuano ya Afrika kwa vijana wenye umri
chini ya miaka 20 itafanyika Jumapili (Mei 11 mwaka huu) saa 10 kamili jioni katika
Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Fainali
hizo za 19 za Afrika zitafanyika mwakani nchini Senegal zikishirikisha timu
saba zitakazofuzu kwenye mechi za mchujo, na Senegal wanaoingia moja kwa moja
kutokana na kuwa wenyeji.
Wakati
Ngorongoro Heroes leo (Mei 9 mwaka huu) saa 10 jioni itafanya mazoezi yake
Uwanja wa Azam uliopo Chamazi, Flying Eagles yenyewe muda huo huo itafanya mazoezi
Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume.
Viingilio
katika mechi hiyo ni sh. 2,000 kwa sehemu zote wakati upande wa VIP itakuwa sh.
5,000. Tiketi zitauzwa uwanjani siku ya mechi katika magari maalumu.
No comments:
Post a Comment