KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Friday, May 9, 2014

Mawazo chanya: Brendan Rogers ni sawa na Bill Shankly 1970 ndani ya Anfiled, wamemkubali

Brendan Rogers akubalika kama
Mnamo mwaka 1971 wakati huo Liverpool ikiwa chini ya meneja Bill Shankly walipoteza taji la FA mbele ya Arsenal.

Lakini pamoja na kulikosa taji hilo meneja huyo kutoka nchini Scotland na kikosi chake kwa ujumla walipongezwa na kupewa zawadi iliyo ambatana na mapokezi makubwa ya kiushujaa.

Ilikuwa ni kama kukubali kwa mashabiki wa klabu hiyo juu ya juhudi kubwa zilizo fanywa na vijana wao katika kulipigania taji hilo.

Kuna mengi ya kufanana na yale yanayotokea msimu huu ambapo 'Reds' wanaonekana kuharibikiwa katika kilele kabisa katika kulisaka taji la na nafasi kubwa ikiwa iko wazi kwa Manchester City.

Mwaka 1971, Shankly aliweka misingi ya zama mpya za mafanikio ambayo alikwenda kwa muda mrefu mpaka alipostaafu.

Tukirudi huko nyuma Shankly alitengeneza timu mpya kufuatia kukivunja kikosi cha wakongwe waliokuwa na umri mkubwa wakiwemo akina Tommy Lawrence, Ron Yeats, Roger Hunt na Ian St John huku wachezaji kama Ray Clemence, Emelyn Hughes, Larry Lloyd John Toshack wakiongezwa.
Why Liverpool must think they are back in 1971
Sanamu ya meneja wa zamani wa Liverpool Bill Shankly ndani yaAnfield
Steve Heighway, Phil Thompson na Kevin Keegan waliongezwa kuanzisha zama mpya za mafanikio kwa wekundu hao wa England.

Ni kama inavyojitokeza sasa huku kioo kiki akisi taswira kuwa Brendan Rodgers ameibadilisha Liverpool kwa kuingiza 'filosofia' ya mpira ya kuwapata nafasi vijana wenye vipaji  ambao watadumu kwa muda mrefu ndani ya Anfield.

Wachezaji kama Philippe Coutinho, Raheem Sterling na Daniel Sturridge wameisukuma Liverpool katika hali ya kuongeza changamoto ya kuwania ubingwa msimu huu ikiwa ni kama alivyofanya meneja muasisi Shankly mwenye heshima kubwa Anfield kwa kuongeza wachezaji wachache wazuri. Hii kuanza upya kwa zama za mafanikio kwa Anfiled.

Kurejea kwao msimu ujao katika ligi ya mabingwa Ulaya kunaweza kuwa mwanzo mzuri wa kipindi cha mafaniki katika klabu hiyo.

Kama ilivyokuwa 1971 mashabiki wanamkubali Brendan Rodgers na wachezaji wake kwa jitihada zao msumu huu na wanaamini kipindi cha kuleta furaha kinaanza.

No comments:

Post a Comment