Kaimu mkufunzi wa timu ya Manchester United nchini
Uingereza, Ryan Giggs amesema kuwa hasikitishwi na hatua ya kumtafuta
kocha mpya wa kilabu hiyo .
Kocha wa timu ya taifa ya Uholanzi Louis van
Gaal ambaye anaitaka kazi hiyo anatarajiwa kuteuliwa kama mrithi wa
aliyekuwa mkufunzi wa timu hiyo David Moyes.
Giggs aliteuliwa kama kaimu kocha wa
kilabu ya Manchester United baada ya Moyes kutimuliwa kutokana na
msururu wa matokeo mabaya mnamo mwezi Aprili.
Wakati huohuo mshambulizi wa kilabu ya
Manchester United Wayne Rooney yuko tayari kuonyesha uhodari wake katika
michuano ya kombe la dunia.
Kulinga na kaimu meneja wa kilabu yake Ryan
Giggs,Rooney ameshindwa kung'ara katika michuano mingi ya kimataifa
tangu alipoanza kusakata soka ya kiwango hicho katika mechi za kuwania
taji la ubingwa wa ulaya mnamo mwaka 2004.
Hatahivyo Giggs ana imani kwamba Rooney ataiwakilisha vyema Uingereza katika dimba la dunia nchini Brazil.
No comments:
Post a Comment