Bingwa mara mbili wa dunia mkenya Asbel Kiprop na
mkenya mwenzake Hellen Obiri walianza msimu wa mashindano ya Diamond
League mjini Doha Qatar kwa kishindo baada ya kushinda mbio zao mtawalia
Ijumaa usiku.
Kiprop alimaliza wa kwanza katika mbio za mita
1,500 kwa dakika 3 sekunde 29. Mwenzake waliyekimbia naye Silas Kiplagat
alimaliza wa pili kwa dakika tatu sekunde 33.
Kwa upande wa wanawake, Obiri, alivunja rekodi ya Afrika ya mbio za mita 3000 baada ya kuzimaliza kwa dakika 8:20.68.
Mkenya mwenzake Mercy Cherono alikuwa wa pili na dakika nane sekunde 21.
Wakenya hao wawili wamekuwa wakimbiaji
waliomaliza mbio hizo kwa kasi zaidi kuliko katika mashindano mengine
yoyote ya Diamond League.
Muethiopia Genzebe Dibaba alimaliza wa sita.
No comments:
Post a Comment