KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Wednesday, June 11, 2014

COASTAL UNION KUFANYA MKUTANO MKUU JUNI 22 MWAKA HUU.

KLABU ya Coastal Union inatarajiwa kufanya mkutano mkuu wa mwaka wa
wanachama utakaofanyika kwenye ukumbi wa Hotel ya Mkonge mkoani Tanga
Juni 22 mwaka huu ambao utakuwa na agenda kuu mbili muhimu zitakazo
jadiliwa na mengineyo.

Akizungumza jana,ofisa Habari wa timu ya Coastal Union,Oscar Assenga alisema
kwenye mkutano huo utakuwa na agenda mbalimbali lakini ya  kwanza
itakuwa ni kupokea taarifa na kujadili taarifa za kazi kutoka kamati
mbalimbali za utendaji ndani ya
klabu hiyo kwa kipindi kilichopita.

Assenga alisema pamoja na hayo lakini kutakuwa na kuthibitisha bajeti
kwa mwaka wa fedha unaofuata baada ya mwaka uliopita kumalizika ambapo
mkutano huo hautaruhusu wanachama wanaodaiwa madeni kuhudhuria.

Aidha alisema pia watafanya marekebisho ya katiba kwa kuongeza kifungu
cha kamati ya maadili ambapo hilo likiwa ni agizo la shirikisho la
soka hapa nchini kwa mujibu wa maelekezo kutoka shirikisho la soka
nchini.

      “Pia tutafanya marekebisho ya katiba kwani tutaongeza kifungu
cha kamati ya maadili ambacho ni muhimu ikiwa ni agizo la shirikisho
la soka nchini (TFF) “Alisema Assenga.

Hata hivyo aliwataka wanachama waliopo sehemu mbalimbali hapa nchini
kuhakikisha wanatimiza haki yao ya msingi kwa kuhudhuria kwenye
mkutano huo muhimu kwa ajili ya maendeleo ya timu hiyo kongwe hapa
nchini.

Mwisho.

ASANTENI NAWATAKIA MAJUKUMU MEMA.
Oscar Assenga.
Ofisa Habari wa Klabu ya Coastal Union,Tanga.

No comments:

Post a Comment