Mtu mmoja amefariki na wengine kujeruhiwa baada ya
sehemu iliyokuwa ikijengwa kuporomoka, katika harakati za kumalizia
ujenzi muhimu wa eneo linaloitwa Monorail, taarifa kutoka Sao Paulo
zimesema.
Ni eneo la kilomita 17 lililokuwa litumike kuunganisha uwanja wa ndege na mfumo wa usafiri wa reli mjini humo.
Brazil imekuwa ikisuasua na sasa inaharakisha kumalizia majengo na miundo mbinu iliyopangiwa kutumika wakati wa kombe la dunia.
Visa vya ajali kuhusiana na ujenzi huo vimekuwa vikiripotiwa mara kwa mara.
Wafanyikazi wanane walifariki wakati wa ujenzi wa eneo la katika la uwanja wa kombe la dunia 'arena'.
No comments:
Post a Comment