Maafisa wa kandanda wa Europa sasa wamemtaka rais wa
shirikisho la kimataifa la kandanda FIFA, Sepp Blatter, ajuzulu kutokana
na madai ya rushwa yanayoindama Fifa.
Wametilia shaka uongozi wake.
Mkuu wa chama cha soka cha uholanzi
Michael Van Praag, amesema chini ya uongozi wa Blatter ,Fifa imeandamwa
na tuhuma za rushwa na ili Fifa kujisafisha ni sharti Blatter angatuke.
Kwa upande wake mwenyekiti wa chama cha soka
Uingereza , Greg Dyke,amesthtumu kauli ya Blatter kuwa madai ya rushwa
kuhusiana na kuchaguliwa kwa Qatar kuwa mwenyeji wa kombe la dunia 2022
yanayoripotiwa katika magazeti ya Uingereza yamechochewa na ubaguzi wa
rangi.
Blatter anatarajiwa kutangaza nia yake ya
kuwania nafasi kipindi cha tano kuingoza Fifa katika uchaguzi wa Fifa
unaotarajiwa kufanyika mwaka ujao.
Kwa sasa wajumbe wa Fifa wanavikao huko Sao
Paulo wakijiandaa kwa ufunguzi wa kombe la dunia hapo kesho ambako Sepp
Blatter pia amekuwa akitoa cheche za maneno dhidi ya wale wanaoisema
vibaya Fifa na Qatar.
No comments:
Post a Comment