Vuguvugu la watu wasio na makaazi nchini Brazil
ambalo limekuwa likiunga mkono maandamano ya kupinga kombe la dunia sasa
wametangaza kuwa wamesitisha maandamano hayo muda wote wa dimba hilo.
Hii ni baada ya kufanikiwa kupata makubaliano na
serikali, hata hivyo bado kuna wasiwasi kwa kuchipuza tena kwa mgomo wa
wafanyakazi wa usafiri wa reli wa mjini uitwao 'Metro' ambao hawajapata
uelewano na serikalii na wametishia kugoma tena kesho hadi pale madai
yao ya nyongeza ya mshahara kwa 12% yatakapotekelezwa.
Kama kweli wakiendeleza vitisho hivyo basi
itakuwa kasheshe kubwa mashabiki kusafiri hadi viwanjani kujionea mechi
walizokuwa wakizisubiri kwa hamu kuu.
Mechi ya ufunguzi hapo kesho ni kati ya wenyeji Brazil dhidi ya Croatia.
Maandalizi ya kombe la dunia ya Brazil yamekubwa
na chelewachelewa na pia migomo ya makundi mbalimbali yanayotumia fursa
hiyo ya kombe la dunia kudai nyongeza za mishahara na huduma bora za
kijamii kutoka kwa serikali inayoshtumiwa kwa ufisadi na matumizi
makubwa katika ujenzi wa viwanja na miundo mbinu kwa ajili tu ya kombe
la dunia.
No comments:
Post a Comment