Thomas Müller na Philipp Lahm wamesaini mikataba mipya itakayowaweka
katikam klabu ya Bayern Munich hadi mwaka wa 2019 na 2018. Wachezaji hao
wako Brazil katika kikosi cha Ujerumani cha Kombe la Dunia.
Mkataba wa nahodha Lahm sasa utakamilika mwaka wa 2018 wakati naye
Müller akisalia katika klabu hiyo kwa miaka mitano ijayo. Wachezaji hao
wawili waliimarika na kupandishwa ngazi kutoka shule ya mafunzo ya
Bayern wakati Lahm akiwa na miamba hao wa Bavaria tangu miaka 11
iliyopita.
Afisa mkuu mtendaji wa Bayern Karl-Heinz Rummenige amesema Lahm na
Mäller ni sehemu muhimu ya Bayern Munich. Wamesalia kuwa waaminifu kwa
klabu hiyo tangu mwanzoni mwa kazi yao ya soka na pia wataendelea
kutekeleza jukumu kubwa katika klabu hiyo bingwa wa Ujerumani.
Kuthibitishwa mikataba ya wachezaji hao wawili kumemaliza uvumi uliodumu
wiki kadhaa kuhusiana na hatima ya mshambuliaji Müller mwenye umri wa
miaka 24 ambaye alikuwa akidaiwa kuihama klabu hiyo.
Müller amekuwa na klabu ya Bayern kwa miaka 14 iliyopita na amesema
uhusiano alio na miamba hao ndio sababu iliyomfanya kusaini mkataba
mpya.
Wachezaji hao wawili wako katika kikosi cha Ujerumani chake Kocha
Joachim Löw kinacholenga kupambana na timu nyingine katika Kombe la
Dunia nchini Brazil na matarajio ya kuleta nyumbani Kombe lao la nne la
dunia.
No comments:
Post a Comment