Mchezaji wa Italy Chiellini akionyesha jeraha alilopata baada ya kung'atwa na Suarez |
Mshambuliaji matata wa timu ya soka ya Uruguay Luis
Suarez anakabiliwa na marufuku ya mda mrefu itakayomlazimu kukosa mechi
nyengine za michuano ya kombe la dunia iwapo atapatikana na hatia ya
kumng'ata mchezaji wa Italy Giorgio Chiellini.
Shirikisho la soka duniani FIFA limeanzisha
harakati za kumuadhibu mcheza huyo kufuatia ushindi wa moja kwa bila
dhidi ya Italy siku ya Jumanne.
Chiellini amedai kwamba Suarez alimng'ata bega lake licha ya Suarez kudai kuwa ni mchazaji huyo aliyemchezea vibaya.
Muonekano wa jeraha la Chiellini |
Suarez mwenye umri wa miaka 27 huenda akapigwa marufuku ya kutoshiriki katika mechi 24 ama miaka miwili.
Refa aliyesimamia mechi hiyo kutoka Mexico Marco
Rodriguez hakuchukua hatua yoyote kufuatia kisa hicho,lakini FIFA bado
inaweza kumuadhibu Suarez.
Aliyekuwa mchezaji wa kiungo cha kati wa timu ya
Liverpool Jan Molby anatarajia kwamba Suarez atapigwa marufuku kwa
mechi zote za kombe hilo zilizosalia.
Raia huyo wa Denmark ameliambia gazeti la
Liverpool la Echo kwamba '' nina hakika FIFA itachukua swala hilo la
Suarez kama mfano kwa wengine''.
''Ni dhahiri kwamba matumaini yake ya kushiriki
katika michuano ya kombe la dunia iliosalia yamekwisha na ninataraji
kwamba FIFA itampatia marufuku ya mda mrefu''.
No comments:
Post a Comment