Kocha wa Italia Cesare Prandeli amesema kuwa
atajiuzulu baada ya mabingwa hao mara nne kubanduliwanje ya Kombe la
Dunia nchini Brazil siku ya Jumanne.
Timu yake ilishindwa kufanya vyema katika mechi za makundi kwa mara ya pili mfululizo katika kombe la dunia.
Italia iliondolewa baada ya kushindwa kwa bao 1-0 na Uruguay katika mechi ya mwisho ya makundi.
“Nilichagua mfumo fulani wa ukufunzi na ndio sababu ninajiuzulu, kwa sababu haukufanya kazi,” alisema.
Aliongezea: “Kuna jambo ambalo limebadilika
tangu nilipotia saini mkataba mpya. Sijui kwanini lakini yameshatukia
ukishikwa shikamana .”
Kocha huyo alitia sahihi mkataba mpya mwezi Mei
iliyopaswa kumpa fursa ya kuhudumu kama mkufunzi mkuu wa Azzurri hadi
baada ya mashindano ya kuwania ubingwa wa bara Uropa Euro ya mwaka wa
2016.
Prandeli amechukua hatua hii baada ya kujiuzulu kwaa rais wa shirikisho la kandanda la Italia Giancarlo Abete.
“Nilizungumza na rais wa shirikisho na naibu wa
rais Demetrio Albertini na nikawapa barua ya kujiuzulu kwangu. Ni jambo
lisilobadilika,”
Licha ya kupoteza dhidi ya Costa Rica katika
mechi yao ya pili, waitaliano walihitaji pointi moja tu ili kufuzu
katika raundi ya muondoano kufuatia ushindi wao wa mechi ya kwanza dhidi
ya Uingereza kwa mabao 2-1.
Lakini bao lake Diego Godin la dakika za mwisho
baada ya Luiz Suarez kuepuka adhabu baada ya kile kinachodhaniwa kuwa
alimng'ata beki wa Italia Girorgio Chiellini, iliwapa Uruguay ushindi na
kuwabandua Italia .
Abete alisema: "Ningependa kutangaza kujiuzulu kwangu.
“Ninaamini kuwa katika mkutano ujao wa bodi wanaweza kumhimiza Cesare kusalia katika nafasi yake.”
No comments:
Post a Comment