Nahodha wa Cameroon Samuel Etoo ana uwezekano wa
kukosa kuchezea nchi yake wikii hii jumatano ,ambapo watachuana na
Croatia kwa sababu ya jeraha analouguza.
Etoo hajafanya mazoezi kwa siku mbili na kuna uwezekano wa kutopona wakati wa kuchezwa kwa mechi hiyo ya group A mjini Manaus
Mshambuliaji huyo mwenye miaka 33
aliandika kauli hii kwenye mtandao wa twitter, " madaktari wana uhakika
kuwa sitaweza kushiriki katika mechi hiyo kwa sababu ya jeraha la goti
linalonisababishaia maumivu.”
Cameroon na Croatia wote walishindwa katika
mechi zao na wanakabiliwa na tishio la kutimuliwa katika kinyang'anyiro
cha kombe hilo la dunia.
Cameroon walicharazwa bao moja kwa nunge walipokutana na Mexico huku Brazil wakiwafunga Croatia mabao matatu kwa moja.
Kukosekana kwa Etoo katika kikosi itakuwa pigo
kubwa kwa Cameroon ambao walishindwa na Mexico hivyo basi inawalazimu
kujikaza ili wasibanduliwe dimbani.
Etoo aliyepata jeraha la goti kwenye mguu wa
kulia mwishoni mwa msimu wake katika kilabu cha Chelsea alisema anatumai
kupata muujiza ili wweze kutetea ushindi wa nchi yake.
Aliongeza kwa kusema, " kama haitafayika
hivyo,nitaendelea kutekeleza wajibu wangu kama nahodha ,hususan kama
kaka mkubwa ili kuongoza wenzangu chipukizi kupata ushindi”
"Kwa muda wa miezi mitatu sijapata nafasi ya
kupata nafuu hata kwa mechi za kukaribia kombe la dunia,sijaweza kufanya
mazoezi kabambe hadi tulipopambana na Ujerumani katika mechi ya
kirafiki.”
"Katika mechi dhidi ya Mexico,nilijaribu kwa
uwezo wangu lakini baada ya kumuona daktari tuligundua nilihitaji
mapumziko ,hata baada ya dakika ya tisa,nilikuwa nahisi uchungu.”
No comments:
Post a Comment