KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Monday, June 16, 2014

MICHAEL SCHUMACHER APATA FAHAMU NA SASA ANAISHI MAISHA YAKE YA KAWAIDA NA FAMILIA YAKE

Schumacher alikuwa anashiriki mchezo wa kuteleza kwa barafu alipoanguka na kuumia vibaya.Schumacher alistaafu kutoka kwa mashindano ya Langalanga mwaka 2012
Mwanamichezo anayefahamika zaidi katika mashindano ya uendeshaji wa magari ya langalanga au F1 Michael Schumacher amepata fahamu.
Michael Schumacher alitoka hospitalini Grenoble na ataendelea kuishi kwa hali yake ya kawaida, zikiwa ni taarifa kutoka ndani ya familia yake.
Michael Schumacher alikuwa akiteleza kwenye theluji kwa skii wakati ajali hiyo ilipotokea.
 
Schumacher alilazimika kudungwa sindano ya kupoteza fahamu baada ya kupata majeraha mabaya kichwani huko French Alps tarehe 29 ya mwezi Disemba mwaka jana.
Madaktari walichukua hatua hiyo ili kusaidia ubongo uliovimba wa mshindi huyo wa mara saba kunywea.
Familia yake iliendelea kwa kushukuru wote waliomtumia jumbe za kumtakia afueni ya haraka kwa kusema zilimtia moyo,pia waliwashukuru madaktari waliomhudumia alikolazwa katika hospitali ya Grenoble,kusini -mashariki mwa ufaransa.


“Michael ametoka hospitalini CHU Grenoble, kuanza safari ndefu ya kurudi katika hali yake ya kawaida. Amepata fahamu,'' Sabine Kehm ambaye ndiye meneja wake alisema katika taaarifa iliyotolewa kwa niaba ya familia yake.
Hapo awali familia yake ilikuwa imeonya kuwa toka mwanzoni itakuwa hali ngumu sana kwa Michael.
Wapelelezi katika ajali hiyo wanasema Schumacher alikuwa kwa mwendo wa kasi kama mwenye uzoefu wa mchezo huo wakati wa ajali hiyo Meribel
Alikuwa akiteleza kwenye theluji alipoanguka na kugonga mwamba.
Schumacher alistaafu kutoka mchezo wa F1 mwaka wa 2012 baada ya kuwa kwa safu hiyo kwa miaka 19.
Alishinda taji mbili na Benetton, mnamo mwaka 1994 na 1995, kabla kuelekea Ferrari 1996 na kupendekeza kupata mataji tano kuanzia 2000

No comments:

Post a Comment