Mwenyekiti wa Yanga Yusufu Manji |
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limepokea malalamiko
kuhusu uamuzi uliofanywa na Mkutano Mkuu wa Yanga uliofanyika Juni Mosi mwaka
huu ambao ulimuongezea muda wa mwaka mmoja mwenyekiti wa klabu hiyo Yusufu Manji kinyume na katiba ya klabu hiyo.
TFF imesema inasubiri muhtasari wa mkutano huo kutoka kwa
uongozi wa Yanga ili tuweze kutoa mwongozo kama ikibidi.
Mwenyekiti wa klabu ya Yanga SC Yusuf Manji aliwaongoza wanachama hai
wapatao 1,560 kupitisha kipengele kipya alichokiita ni kwa ajili ya maslahi na
faida ya Wana Yanga kwani bila kufanya hivyo timu isingeweza kuruhusiwa
kushiriki Ligi Kuu msimu ujao.
Aidha
katika mkutano huo Manji aliwatoa hofu wanachama kwa kuwaambia kuwa
usajili unaendelea kufanyika na nafasi zilizobakia ni nne tu hivyo pindi
utakapokamilika basi wataweka wazi kila kitu.
No comments:
Post a Comment