KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Monday, June 16, 2014

Louis van Gaal kumpeleka Thomas Vermaelen Old Trafford

Mlinzi Thomas Vermaelen
Imeripotiwa kuwa Thomas Vermaelen amekubali mpango wa kujiunga na Manchester United akitokea Arsenal msimu ujao.
Mlinzi huyo raia wa Belgiam ambaye anamtumia wakala mmoja na mshambuliaji wa kimataifa wa Uholanzi Robin van Persie, amekosa mvuto ndani ya washika mitutu wa London na ameamua kujiimarisha kikazi ndani ya ngome kongwe.

Bosi mpya wa United Louis van Gaal anasaka walinzi wazoefu kuimarisha kikosi kufuatia kuondoka kwa Nemanja Vidic na Rio Ferdinand ambapo anaamini kuwa mholanzi Vermaelen anauwezo wa juu kuziba pengo hilo.

 
Akiwa na umri wa miaka 28 na akiwa amesaliwa na mwaka mmoja wa mkataba wake na Arsenal, inaaminika kuwa maamuzi ya Vermaelen kumaliza mkataba wake wa miaka mitano na Gunners utamfanya apokee kiasi ya pauni £100,000 kwa wiki katika klabu ya Manchester United.
Van Gaal atalazimia kukubali ada isiyopungua pauni milioni £10 kutoka kwa Arsenal.