KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Tuesday, June 10, 2014

HUKUMU YA MICHAEL WAMBURA KUTANGAZWA KESHO, HARUFU YA USHINDI NA MWANGA WAMUANGAZIA

Uamuzi kuhusu rufani ya Michael Wambura kupinga kuenguliwa kugombea urais wa Rais utatangazwa kesho (Juni 11 mwaka huu) saa 6 kamili mchana na Mwenyekiti wa Kamati ya Rufani ya Uchaguzi ya TFF, Wakili Julius Lugaziya.
Chanzo cha habari cha kuaminika  kabisa kikiongea na mtandao wa Rockersposts kimesema kuwa kamati ya rufani ya TFF imemrejesha Wambura katika kinyang'anyoro hicho na kwamba taarifa kamili ya maamuzi hayo na kuendelea kwa mchakato wa uchaguzi wa Simba itatolewa hapo kesho.

Wambura aliondolewa katika kinyang'anyiro hicho na kamati ya uchanguzi ya klabu hiyo iliyo chini ya wakili Dr Damas Ndumbaru kutokana na kusimamishwa uanachama wake May 5 mwaka 2010 kufuatia kuipeleka klabu hiyo mahakamani akifungua kesi nambari 100.