KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Tuesday, June 10, 2014

Kiungo Jordan Brian Henderson kumshurutisha kocha mkuu Roy Hodgson ili ampe nafasi kombe la dunia

Kiungo wa klabu ya Liverpool Jordan Brian Henderson amesema hana budi kupambana katika mazoezi ya timu ya taifa ya Uingereza kwa lengo la kumshurutisha kocha mkuu Roy Hodgson ili amujumuishe katika kikosi cha kwanza kitakachecha mchezo wa ufunguzi wa kundi la nne katika fainali za kombe la dunia huko nchini Brazil dhidi ya timu ya taifa ya Italia.

Jordan Henderson amesema hana budi kufanya hivyo kutokana na viwango vya ubora kwa wachezaji wote wa timu ya taifa ya Uingereza kushabihiyana.

Amesema kila mmoja anahitaji kucheza mchezo huo wa ufunguzi kutokana na umuhimu wa kutaka kuisaidia timu ya taifa la Uingereza hivyo kwa sasa anajitahidi kwa lengo moja tu, la kuhitaji kuwa sehemu ya kikosi cha kwanza siku ya jumamosi.

Hata hivyo kiungo huyo bado amesema endapo itatokea kinyume na matarajio yake ya kushindwa kuwa sehemu ya kikosi cha kwanza kitakachocheza mchezo dhidi ya timu ya taifa ya Italia, ataichukulia hali hiyo kama changamoto ambayo itamuongezea chachu ya kufanya mazuri zaidi mazoezini ili malengo yake yatimie.

Kikosi cha timu ya taifa ya Uingereza jana kimefanya mazoezi kwa mara ya kwanza nchini Brazil katika uwanja wa jeshi uliopo mjini Rio de Janeiro.