Shambulizi la hivi karibuni kukumba Kenya ni la Mpeketoni ambapo watu zaidi ya sitini waliuawa |
Serikali ya Kenya imewataka raiya kuwa waangalifu na kuwatahadharisha wakati huu wanapotazama michuano ya kombe la dunia.
Waziri wa usalama Joseph Ole Lenku amewataka
wananchi kutazama mechi hiyo nyumbani kwao badala ya mikahawani ili
kuzuia uwezekano wa kushambuliwa na wahalifu.
Hii ni baada ya kutokea mashambulizi kadhaa nchini humo na kuzorotesha hali ya usalama.
Jumapili usiku watu wasiojulikana na ambao
walikuwa wamejihami walishambulia wakazi wa mji wa Mpeketoni eleo la
Lamu Pwani ya Kenya na kusababisha vifo vya watu 60.
Wakazi hao walishambuliwa wakiwa wanatazama michuano ya kombe la dunia mikahwani na watu waliokuwa wamejihami kwa silaha nzito.
Malumbano yalizuka miongoni mwa wanasiasa punde
baada ya mashambulizi hayo kuhusu nani aliyeyatekeleza hata baada ya Al
Shabaab kukiri kuyafanya.
Shambulizi la kwanza lilitokea karibu na Lamu
lilifanyika Mpeketoni wakati baadhi ya mashabiki wa soka walikuwa
wakitazama mechi ya kombe la dunia.
'Tahadhari ya kwanza ''
Tangu wakati huo idara ya ulinzi ya Marekani
imesisitiza kuhusu tahadhari kwa raia wake kusafiri katika eneo la pwani
kwa kuhofia matukio sawa na hayo.
Ni mara ya kwanza kwa serikali ya Kenya
kuwashauri raiya wake kutoenda katika maeneo ya umma ya kutazamia kombe
la dunia na kuwataka wafanye hivyo nyumbani kwao.
Wakenya wengi huenda katika mikahawa kutazama mechi na ushauri huu huenda ukawakera wengi.
Taarifa hiyo inadai kuwa serikali imeimarisha
usalama katika sehemu nyingi nchini mbali na kuwaagiza wamiliki wa mabaa
na mikahawa kuchukua tahadhari za kiusalama ili kujiepusha na balaa.
Ushauri huo unatolewa wakati serikali nyingi
zikijumuisha Marekani na Uingereza zimewatahadharisha raiya wake
kusafiri katika maeneo yanayopakana nan a Somalia, Mombasa na baadhi ya
sehemu za Nairobi.
Miaka minne iliyopita nchini Uganda Zaidi ya
watu 70 walifariki katika shmbulizi walipokuwa wakitazama kombe la dunia
na serikali ya nchi hiyo imechukua tahadari za kiusalama ili kuzuia
marudio ya matukio kama hayo.
No comments:
Post a Comment