KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Friday, June 20, 2014

Tanzia: Kolo na Yaya Toure wapatwa na msiba mkubwa wa mdogo wao Ibrahimu mshambuliaji wa Al Safa SC ya Lebanon

Wachezaji ndugu wa Ivory Coast  Yaya Toure na Kolo Toure wako katika majonzi makubwa ya kuondokewa na mdogo wa Ibrahim Toure.
Taarifa za kufariki dunia kwa ndugu yao huyo wamezipata baada ya mchezo ambao Ivory Coast walichapwa bao 2-1 na Colombia jana Alhamisi. 
 Imethibitshwa na chama cha soka cha nchi hiyo leo asubuhi ambayo ilituma salamu za pole kwa ndugu hao.
Taarifa ya chama hicho imesomeka
"Kolo na Yaya Toure wamepata msiba wa kufariki mdogo wao Toure Oyala Ibrahim. Taifa zima na ujumbe mzima wa kikosi cha timu ya taifa ungependa kuungana nao kwa kila namna katika kipindi hiki kigumu kwao."
“Rais wa FA ya Ivory Caost na kamati nzima ya utendaji inatangaza kwa masikitiko msiba huu wa familia ya mpira kufuatia kufariki kwa M.Toure Oyala Ibrahim, mdogo wa Toure Kolo Abib na Toure Yaya Gnegneri, ambao umetokea tarehe 19 June katika mji wa Manchester (England).”
Ibrahim amekuwa akiishi nchini Lebanon ambako alikuwa akiichezea klabu ya Al Safa SC katika nafasi ya ushambuliaji.