Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF),
Jamal Malinzi amewataka makocha wa mpira wa miguu wafanyie kazi kwa vitendo
mafunzo wanayopata badala ya kuweka makabatini maarifa waliyopata.
Akifunga rasmi mafunzo ya wiki mbili ya makocha wa
mpira wa miguu ya Leseni B inayotambuliwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu
Afrika (CAF) jijini Dar es Salaam leo (Juni 20 mwaka huu), Rais Malinzi
amewataka makocha hao kuwapa mafunzo ya awali (basic) walimu wa shule za msingi
kwa vile TFF ina mpango wa kuhakikisha kila shule ya msingi nchini inapata
mipira kumi kila mwaka.
“Kila mwaka tutakuwa na mashindano ya kitaifa ya
watoto wenye umri chini ya miaka 13 kuanzia mwaka huu. Hivyo ninyi makocha huko
mnaporudi muwafundishe walimu wa shule za msingi mafunzo ya awali ya ukocha,”
alisema.
Kozi iliyohudhuriwa na makocha 26 kutoka Tanzania Bara
na Zanzibar ilikuwa chini ya Wakufunzi wa CAF, Honour Janza kutoka Zambia, na
Sunday Kayuni na Salum Madadi wa Tanzania. Janza pia ni Mkurugenzi wa Ufundi wa
Chama cha Mpira wa Miguu Zambia (FAZ).
Makocha walioshiriki kozi hiyo ni Abdalla Mohammed
Juma (Zanzibar), Abdul Banyai (Temeke), Abdul Nyumba (Temeke), Abdulmutik Haji
(Zanzibar), Aley Mohammed (Zanzibar), Ali Vuai Shein (Zanzibar), Dennis Kitambi
(Morogoro), Dismas Haonga (Ilala), Emmanuel Massawe (Shinyanga), Fikiri Elias
(Arusha), Fulgence Novatus (Mwanza), Hababuu Ali Omar (Zanzibar), Juma Mgunda
(Tanga) na Kidao Wilfred (Ilala).
Wengine ni Maka Mwalwisi (Mbeya), Malale Hamsini Keya
(Zanzibar), Mecky Maxime (Morogoro), Mohammed Tajdin (Temeke), Mussa Furutuni
(Dodoma), Nassor Salum Mohamed (Zanzibar), Peter Mhina (Ruvuma), Said Mohamed
Abdulla (Zanzibar), Salim Makame (Zanzibar), Salum Ali Haji (Zanzibar), Sebastian
Nkoma (Ilala) na Wane Mkisi (Dar es Salaam).
No comments:
Post a Comment