KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Friday, June 13, 2014

Usajili: Alex Song kuungana na Diego Costa na Cesc Fabregas darajani

Chelsea wameanza mpango mwingine wa kumsajili kiungo wa Barcelona ambaye pia ni mchezaji wa zamani wa Arsenal Alex Song.
Meneja Jose Mourinho tayari amemuweka katika rada yake kwa lengo la kuimarisha sehemu ya kiungo cha klabu hiyo.
The Blues jana walithibitisha ujio wa kiungo wa zamani Arsenal Cesc Fabregas kwa uhamisho uliogharimu pauni milioni £27 akitoke kwa Barcelona na sasa wanaonekana bado hawajamaliza zoezi hilo.
Song mwenye umri wa miaka 26, naye kama ilivyokuwa kwa Fabregas alipewa kauli ya kukatisha tamaa kutoka uongozi wa klabu yake ikisema kuwa anaweza kuondoka kiangazi hii kwa pauni milioni £10 na tayari Chelsea wamefungua mazungumzo ya mpango wa uhamisho wake.
Mourinho anasaka kiungo mchezeshaji atakaye chukua nafasi ya John Obi Mikel, ambaye amewekwa kwenye mnada wa klabu hiyo na hivyo kuongeza mchezaji kiungo mwenye ushindani wa Nemanja Matic.
Song anaonekana kama ni mtu anayefanana na wazo hilo na taarifa kutoka nchini Hispania zinaarifu kuwa Chelsea wanamatumaini watafanikiwa kumchukua wiki zijazo.

Song anatarajiwa kung'aa akiwa na kikosi cha Cameroon katika fainali za kombe la dunia nchini Brazil.