KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Tuesday, July 1, 2014

Abdulhalim Humoud kutoka Simba, Crispine Odulla (Coastal Union) na Haji Ugando (Mbagala Market FC) kujiunga na Sofapaka na Bandari za Kenya

Abdulhalimu Humud
Wachezaji watano wameombewa Hati ya Uhamisho ya Kimataifa (ITC) ili waweze kucheza mpira wa miguu nchini na nje ya Tanzania.

Abdulhalim Humoud kutoka Simba, Crispine Odulla (Coastal Union) na Haji Ugando (Mbagala Market FC) wameombewa ITC na Shirikisho la Mpira wa Miguu la Kenya (FKF) ili wakacheze nchini humo katika klabu za Sofapaka, Bandari FC na Nakuru All Stars.

Vilevile TFF imemuombea ITC mchezaji Ismaila Diarra kutoka nchini Mali ili aweze kujiunga na timu ya Azam FC. TFF inafanyia kazi maombi hayo, na mara taratibu zote zitakapokamilika itatoa ITC hizo kwa wachezaji wanaokwenda nje ya Tanzania.