KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Tuesday, July 1, 2014

MARCIO MAXIMO AWACHANA WACHEZAJI WAKE LIVE NA KUWEKA WAZI MIPANGO YAKE KWAO IKIWA NI PAMOJA NA KUWAONGEZA WACHEZAJI 10 WA VIJANA

Kocha mkuu wa Yanga Marcio Maximo akiwa na msaidizi wake Leonado Neiva
 Kocha mkuu wa klabu ya Yanga Marcio Maximo mapema jana asubuhi alikutana kwa mara ya kwanza na wachezaji wote  watakao itumikia klabu hiyo kwenye michuano ya ligi kuu ya Vodacom msimu ujao katika makao makuu ya klabu hiyo yaliyoko katika makutano ya mitaa ya Twiga na Jangwani.
Mbali ya wachezaji hao wa kikosi cha kwanza ukiachana na wale walioko katika vikosi vya timu za taifa  pia Maximo aliwajumuisha wachezaji wa kikosi cha pili cha wenye umri chini ya umri wa miaka 20.
Katika kikao hicho kilichofanyika kwenye makao makuu ya klabu hiyo mitaa ya Twiga na Jangwani asubuhi ya leo maximo amewaambia wachezaji hao lengo la kikao hicho mbali ya kufahamiana, lakini pia alikuwa akitaka kuweka wazi mipango yake kwa wachezaji hao kabla ya kuanza rasmi mazoezi.
Kwa mujibu wa taarifa za ndani toka kwa mmoja wa wachezaji wa klabu hiyo aliyekuwepo kwenye kikao hicho ameiambia Rockersports kuwa  jambo la kwanza alilolisisitiza mbrazil huyo kwa wachezaji ni suala zima la nidhamu.
Amesema kwake nidhamu ni kitu cha kwanza na asingependelea  kuona wachezaji wa Yanga hasa anaowafundisha wakikosa nidhamu na kusisisitiza kuwa kamwe hatomuonea huruma mchezaji ambaye hana nidhamu kwani bila nidhamu hakuna chochote atakacho weza kukijenga ndani ya kikosi cha timu hiyo.
Aidha mbrazil huyo amewambia wachezaji hao kuwa kikubwa anachokiomba kwao ni ushirikiano mkubwa kwani bila wachezaji hao kumpa ushirikiano hakuna kitakachofanikiwa.
Aidha kocha huyo amewaambia wachezaji wake kuwa kila mpenzi wa Yanga kwa sasa anaamini kuwa ujio wake ndani ya klabu hiyo kama kocha utabadilisha mwenendo wa kiuchezaji na kuleta matokeo mazuri na kwamba Yanga itakuwa timu ya kutisha barani Afrika na katika ligi kuu Tanzania barana Afrika kwa ujumla.
Amewataka wachezaji hao kutambua kuwa yeye ni kocha mwenye jina kubwa na amejijengea jina sehemum mbalimbali ikiwemo Tanzania hivyo wengi wanamuangalia kwa jicho la tatu kuwa nini atakifanya ndani ya klabu hiyo.
Amesema matokeo mazuri na mafanikio kwa pande zote tatu yaani yeye kama kocha, wachezaji wenyewe pamoja na klabu yatapatikana endapo tu wakifanikiwa kushirikiana na kujituma na kila mmoja kutimiza wajibu wake na kwamba hakuna miujiza nyuma ya hilo na wao kufuata kile anachokifundisha.
Maximo amezungumza mengi ikiwa ni pamoja na kuelezea mipando yake na vipaumbele mbalimbali ikiwemo kuwatumia wachezaji wa kikosi cha pili cha under 20 ambapo amedhamiria kuwajumuisha wachezaji 10 kutoka kikosi hicho ili kuongeza nguvu pia akawaambia wachezaji hao kuwa katika mipango yake ameweka kipaumbele zaidi katika kutumia wachezaji vijana na kusema katika kikosi chake angependelea zaidi kuwa na wachezaji vijana ili kupata kikosi mchanganyiko.
Kuhusu ratiba ya mazoezi Maximo ametoa ratiba nzima ya kipindi maandalizi ya msimu ujao ikiwa ni pamoja na kufanya mazoezi mara mbili kwa siku asubuhi na jioni mazoezi ambayo yatahusisha ufukweni , GYM pamoja na viungo lakini pia masuala ya kiufundi japo kidogo katika siku za mwanzoni.
Alitumia kikao hicho kumaliza na kuzika tofauti zake na Juma kaseja kwa kueleza kinaga ubaga kuwa kwasasa amefungua ukurasa mpya na kipa hiyo akisema kuwa kuwa hana kinyongo tena na Kaseja na kwamba yale yalikuwa ni kipindi kile cha timu ya taifa na kwamba Kaseja kwake ni mchezaji mpya akiamini Kaseja ataonyesha ushirikiano mkubwa kwake.


Yanga imeanza mazoezi asubuhi hii  katika fukwe za bahari ya Hindi eneo la Coco Beach kabla ya jioni kuendelea na mazoezi hayo uwanja wa bandari.

No comments:

Post a Comment