Andrey Coutinho akisaini mkataba wa kuitumikia Yanga kwa kipindi cha miaka miwili mbele ya Katibu Mkuu Beno Njovu leo makao makuu ya klabu |
Kiungo mshamabuliaji Andrey Marcel Ferreira Coutinho raia wa Brazil
leo amesaini mkataba wa miwili kuitumikia timu ya Young Africans kwa
ajili ya michuano mbalimbali ikiwemo ya Ligi Kuu ya Vodacom pamoja na
mashindano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika.
Katibu mkuu wa Young Africans Bw Beno Njovu amesema usajliwa
mchezaji Coutinho ni sehem ya muendelezo wa maandalizi ya msimu mpya wa
Ligi Kuu na kama ilivyokawaida wao mambo yao ni kimyakimya.
Coutinho
ambaye alizaliwa tarehe 12 Januari 1990 amekulia kwenye mji wa Berem
ambapo alianza kucheza soka la kulipwa katika klabu ya Paysandu Sports
Club kabla ya kwenda nchini Asia katika nchi ya Myanmar katika klabu ya
Rukhapura United.
Mpaka anajiunga na klabu ya Young Africans
Andrey Coutinho alikuwa akichezea timu ya Castanhal EC iliyopo kwenye
Ligi Daraja la pili ambao aliweza kuichezea kwa michezo yote ya
mzunguko wa pili mwaka 2014.
Katika hatua nyingine kikosi cha
Young Africans kinatarajia kuendelea na mazoezi kesho chini ya kocha
Marcio Maximo katika ufuke wa Coco Beach ikiwa ni siku yake ya kwanza na
jioni katika Uwanja wa Bandari Tandika kuanza kazi baada ya leo kuwa na
mkutano wa ndani na wachezaji wake pamoja na benchi la ufundi.
No comments:
Post a Comment