Algeria iliyoingia kwa
mara ya kwanza katika hatua hiyo ya 16 bora itakuwa inataka kuendeleza
ubabe wake kwa Ujerumani ambayo ilikubali kichapo katika michezo miwili
iliyowahi kukutana na mbweha hao wa jangwa.
Kocha wa Algeria Vahid Halilhodzic amesema ushindi mwaka 1982 utachangia
kuwapa nguvu na ujasiri wachezaji wake katika mchezo wa leo huku
Joechim Loew akisema kuwa mchezo huo hauna maana yoyote kwa wachezaji wa
sasa kwakua wengi wao walikuwa hawajazaliwa.
Washindi katika michezo ya leo, watakutana katika hatua ya robo fainali
ya kombe la dunia ambayo itaanza kuchezwa tarehe 4 ya mwezi huu.
No comments:
Post a Comment