KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Monday, June 30, 2014

Ryan Giggs: Sikuwa tayari kuwa mkufunzi

Ryan Giggs: Sikuwa tayari kuwa mkufunzi
Aliyekuwa kaimu kocha na Mchezaji wa Manchester United Ryan Giggs amekiri kuwa hakuwa tayari kwa majukumu ya kazi kama kocha wa klabu hiyo ya Uingereza.
Giggs anasema kuwa uteuzi huo ulikuwa mapema kuliko alivyotarajia.
Giggs alichukua hatamu kama kaimu kocha mwisho wa msimu uliopita baada ya kocha David moyes Kutemwa kufuatia msururu wa matokeo duni tangu achukue hatamu Old Trafford.
Giggs aliyekuwa kocha katika mechi nne za mwisho alitwaa ushindi katika mechi 1 akashindwa moja na kisha akatoka sare katika mechi ya mwisho Manchester united ilipomaliza msimu katika nafasi ya 7 .
Giggs aliyasema hayo alipokuwa akikamilisha kozi ya ukufunzi akijitayarisha kusaidiana na Louis van Gaal Old Trafford .
Giggs alistaafu kama mchezaji msimu uliopita baada ya kuiwakilisha Man united katika mechi 963 na kufunga mabao 168 .