Kocha Vahid Halilhodzic amesema swala kufunga au la ni la kibinfasi |
Kocha wa timu ya taifa ya Algeria ambayo inashiriki
kombe la dunia nchini Brazil, Vahid Halilhodzic amekataa kufichua idadi
ya wachezaji wake ambao wanafunga mfungo wa Ramadhan kabla ya mechi yake
na Ujerumani baadaye Jumatatu
Mfungo huo ambao ni wa siku 30 ilianza Jumapili
na kocha Halilhodzic, mwenye umri wa miaka 61, alikataa kujibu swali
ikiwa wachezaji wake watafunga Ramadhan au la wakati wakicheza.
"hili ni swala la kibinafasi na
unaponiuliza swali hilo basi unaonekana kukosa nidhamu na heshima, ''
alijibu kocha huyo raia wa Bosnia.
"wachezaji watafanya watakavyo na sitaki kuzungumzia swala hili tena. ''
Mfungo wa Ramadhan ni sharti kwa kila muisilamu
na ni moja ya nguzo za imani yua dini ya kiisilamu, ingawa wagonjwa na
wazee wanaruhusiwa kutofunga.
Watu ambao wanasafiri au kuenda vitani pia
wanaruhusiwa kujiepusha na kufunga na hii ni moja ya sababu ambazo
wanamichezo hukosa kufunga hadi wanapokamilisha shughuli zao.
Wachezaji wa Algeria baada ya ushindi wao katika kundi H
Bila shaka ni swali ambalo lilimuudhi kocha
Halilhodzic. ''Nimesoma katika baadhi ya magazeti nchini Algeria
yakinikosoa na kunichafulia jina.Wanajaribu kuzua chuki kwa familia
yangu , kwangu mimi na hili linanichukiza sana, '' alisema kocha huyo
kwa hasira.
"sio mara ya kwanza kwangu kuwa na wachezaji
waisilamu katika timu ya mpira. Mimi mwenyewe ni Muisilamu na mimi
huwaacha kuwa huru wachezaji kuamua wanachotaka. Hili ni swala la
kibinafsi. ''
"kwa wale wanaoendelea kukosoa timu hii na
wachezaji nadhani ni jambo la aibu sana. Lakini nitaendelea kuwa na
wachezaji hawa, na ni jambo la kusikitisha kuwa mnaendelea kukosoa timu
yangu kila wakati. ''
Kinara wa timu hiyo, Madjid Bougherra, ameeleza
kuwa atafunga ingawa mchezaji wa Ujerumani Mesut Ozil na mchezaji wa
Ufaransa Bacary Sagna ambao ni waisilamu wamesema hawatafunga.
No comments:
Post a Comment