KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Tuesday, July 1, 2014

Cameroon yadaiwa kupanga mechi Brazil

Maafisa wa Cameroon watapelelezwa kutokana na madai kwamba saba kati ya wachezaji wa timu ya taifa hilo walihusika katika kupanga mechi katika Kombe la Dunia linaloendelea nchini Brazil.

Kamati ya maadili ya shirikisho la kandanda la taifa hilo litachunguza shutuma za "udanganyifu" wa "wachezaji saba wabaya" katika mechi zao tatu za makundi.

Madai hayo yametolewa na gazeti moja la kijerumani na mtu aliyehukumiwa kwa kuhusika na kupanga mechi nchini Singapore.

Cameroon ilipoteza mechi zote za kundi A, ikiwemo ile waliolazwa na Croatia kwa mabao 4-0.

Mchezaji wa 'The Indomitable Lions' Alex Song, alionyeshwa kadi nyekundu kwa kumgota Mario Mandzukic mgongoni katika mechi hiyo, huku wachezaji wenzake Benoit Assou-Ekotto na Benjamin Moukandjo wakizozana baadaye katika mechi hiyo.

Ripoti kutoka katika shirikisho la kandanda la Cameroon lilisema: "Madai yaliyotolewa majuzi kuhusu udanganyifu katika mechi tatu za mwanzo za Cameroon katika Kombe la Dunia la 2014, hasa kati ya Cameroon na Croatia, na vile vile 'kuwepo na wacheza saba wabaya katika timu yetu ya taifa' hayaambatani na maadili na kanuni zinazopendekezwa na usimamizi wetu, pamoja na kanuni za Fifa na maadili ya taifa letu.

"Tuna nia kuu ya kutumia mbinu zote zinazostahili ili kutatua swala hili linalosumbua kwa muda mfupi iwezekanavyo."

'FIFA yataka uchunguzi wa wazi'

Fifa haikusema iwapo ilikuwa ikichunguza swala hilo au la, kwani bodi hiyo inayosimamia kandanda ulimwenguni "ilitaka uchunguzi uwe wazi".



Wachezaji wa Cameroon wakichapana katika mechi yao uwanjani


Hata hivyo, iliongezea kuwa: 
"kwa ujumla, uadilifu katika mchezo huu ndio swala linalopewa kipaumbele na Fifa, kwa hivyo, tunatilia madai yoyote kuhusu udanganyifu maanani sana."


'Mgogoro wa marupurupu'

Matayarisho ya Cameroon kabla ya michezo hiyo nchini Brazil yalitatizika baada ya wachezaji kukataa kupanda ndege kuelekea Brazil hadi wakati mgogoro uliohusiana na wachezaji hao kulipwa marupurupu yao ulipotatuliwa.

Maelewano ya fedha hatimaye yalifikiwa na shirikisho la kandanda la Cameroon, Fecafoot, lakini safari ya kikosi hicho kuelekea Brazil ilikuwa imecheleweshwa kwa takriban siku nzima.

Walianza michezo hiyo kwa kushindwa kwa bao 1-0 na Mexico kabla ya kulazwa na Croatia na wenyeji Brazil waliowafunga mabao 4-1.

"Wachezaji kadhaa walikosa nidhamu, na ndio sababu tumefungwa mabao manne," mkufunzi wa Cameroon Volker Finke aliambia gazeti la kifaransa la L'Equipe baada ya kushindwa na Croatia.

"Ninajua ni vigumu kucheza na wachezaji kumi, lakini hilo si sababu ya kupoteza katika mkondo huu.

"Mechi ilikuwa sawa hadi tulipoonyeshwa kadi nyekundu. Wacroatia walifanya vizuri mbele ya lango lakini Cameroon pia ilikuwa na nafasi ya kufunga.

"Tabia ya wachezaji kadhaa kwa kweli sio nzuri. Hata tulipokuwa bado na wachezaji 11 kila upande, haikuwa ya kupendeza."

No comments:

Post a Comment