KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Wednesday, July 2, 2014

Frank Domayo afanyiwa upasuaji na atakuwa nje ya uwanja wa miezi minne

Kiungo wa Azam Domayo atakuwa nje ya uwanja miezi minne
AZAM FC imesema kiungo wake Frank Domayo atakuwa nje ya uwanja wa muda wa miezi minne kufuatia upasuaji wa mguu aliofanyiwa nchini Afrika kusini hapo jana.

Akiongea na Rockersports afisa habari wa Azam fc Jafari Iddi Maganga amesema uchunguzi wa afya wa kiungo huyo aliofanyiwa na mganga mkuu wa klabu hiyo Dr Mwamkemwa ulibaini kuwa Domayo ana matatizo ya msuli wa mguu wake wa kushoto na kwamba atatakiwa kufanyiwa upasuaji.

Uongozi wa Azam fc wiki iliyopita ulimpeleka Domayo nchini Afrika kusini akiambatana na Dr Mwankemwa ambapo jana alifanyiwa upasuaji katika hospitali ya Vicent Parent na imeelezwa kuwa anaendelea vizuri huku akitarajiwa kurejea nchini Jumapili.

 Jafari Iddi Maganga amesema kiungo huyo atakuwa nje ya uwanja kwa kipindi miezi minne akiendelea kupata tiba na uangalizi wa karibu wa jeraha lake kabla ya kurejea uwanjani kuitumikia klabu yake hiyo mpya ambayo amejiunga nayo hivi karibuni.