KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Wednesday, July 2, 2014

Rais wa ZFA Idarous aupongeza uongozi mpya wa Simba

Rais wa ZFA Ravia Idarous
Chama cha soka cha Zanzibar ZFA kimeupongeza uongozi mpya wa klabu ya Simba uliochaguliwa Jumapili katika ukumbi wa bwalo la maafisa wa polisi Oysterbay jijini Dar es Salaam.
 
Akioungea na Rockersports Rais wa ZFA Ravia Idarous amesema yeye pamoja na chama chake ZFA wanafahamu vema kuwa klabu ya Simba ni moja kati ya vilabu vikubwa hapa nchini, na kwamba kumalizika kwa uchanguzi wa klabu hiyo na kupatikana kwa viongozi wake wapya kwa mujibu wa klabu katiba ya klabu hiyo ni jambo la kupongezwa sana kwani Simba ni klabu ya wanachama na hivyo kila mwanachama anakuwa na utashi wake na maslahi tofauti na kwamba hilo pekee linatosha kulipa hongera.
 
Idarous amesema ZFA itakuwa bega kwa bega na uongozi huo mpya ambao umeandika historia ya kuongozwa na Rais kwa mara ya kwanza na kwamba ZFA inawakaribisha viongozi hao huko Zanzibar kwani klabu hiyo ina wanachama wake wengi na ambao wangependelea kuwaona viongozi wao visiwani huko.

No comments:

Post a Comment