Hans Poppe kuendelea kuongoza kamati ya usajili Simba |
Rais mpya wa klabu ya Simba Evance Elieza Aveva amemteua
Zacharia Hans Poppe kuendelea kuwa mwenyekiti wa kamati ya usajili ya klabu
hiyo, huku Makamu wake akiwa ni Kassim Mohammed Dewji.
Akizungumza na Waandishi wa Habari kwa mara ya kwanza tangu kuchanguliwa kuwa Rais wa kwanza wa klabu hiyo juma lililopita kwenye bwalo la maafisa wa polisui
Oysterbay jijini Dar es salaam, Aveva amesema uteuzi huo umepewa Baraka na
kamati yake ya utendaji ambayo jana ilifanya kikao chake cha kwanza.
Amewataja wajumbe wengine wa kamati hiyo kuwa ni Said Tuliy, Musley Al Ruwaih, Crescentius Magori na Dk Roadney Chiduo.
Aveva ametumia kifungu cha ibara ya 28 ya katiba ya Simba ambayo inampa mamlaka Rais wa klabu ya Simba kuteua wanchana watano kuingia katika kamati ya Utendaji ya klabu hiyo ambapo Aveva ameteua wanachama watatu kwanza huku akiacha wazi nafasi mbili ambazo zitajazwa baadaye.
Wajumbe hao ni Mohamed Nassor, Musleh Al Ruwaih na Salim Abdallah.
Aveva ametangaza kuundwa kwa kamati ya Mashindano ambayo itaongozwa na mwenyekiti Mohammed Nassor, makamu wake atakuwa Iddi Kajuna ambapo wajumbe wengine ni Jerry Yambi, Hussein Simba na Mohammed Omar.
Aveva
pia ametangaza kamati ya soka la vijana ambayo itakuwa chini ya mwenyekiti, Said Tuliy, Ally Suru, Patrick Rweyemamu, Mulamu Nghambi,
Madaraka Suleiman na Amina Poyo.
Aidha Rais huyo wa Simba Evance Aveva amesema kikao cha kamati
ya utendaji kilichokutana jana kimeamua kuwasimamisha uanachama, wanachama 69 waliokwenda
Mahakamani kupinga uchaguzi wa klabu hiyo mwishoni mwa mwezi uliopita.
Michael wambura kujadiliwa na wanachama Agosti 3 |
Amesema hatima ya wanachama hao, pamoja na ya mwanachama
mwingine maarufu, Michael Wambura aliyeenguliwa kwenye uchaguzi kwa kosa kama
hilo, itaamuliwa katika Mkutano Mkuu Agosti 3, mwaka huu.
Pia amesema mkutano huo wa Agosti utapitia mabadiliko ya katiba kwa kuwa mkutano huo ni wa kawaida wa wanachama.
No comments:
Post a Comment