KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Sunday, July 13, 2014

Liverpool yakamilisha usajili wa mchezaji wa nne, mara hii ni Lazar Markovic wa Benfica

Lazar Markovic
Hatimaye Lazar Markovic amekamilisha uhamisho wake wa kujiunga na Liverpool kwa ada ya pauni milioni £19.8 akitokea Benfica na kutuma ujumbe kwa mashabiki wake kupitia ukurasa wake wa Facebook.
Winga huyo mwenye umri wa miaka 20 ambaye alikuwepo Merseyside hapo jana kumalizia mambo kadhaa ikiwemo mambo binafsi ametupia katika ukurasa wake huo ujumbe ambao umeonyesha wazi kuwa hatarejea tena Estadio da Luz msimu ujao.
‘Ahsante kwa kila kitu na kwaherini!’ huo ni ujumbe ambao ameutuma asubuhi ya leo ambao uliambatana na picha yake akiwapungia mashabiki.
Anakuwa ni mchezaji wa nne wa kiwango cha juu kusajiliwa na Liverpool kiangazi hii akitanguliwa na Rickie Lambert, Adam Lallana na Emre Can.