Kocha wa Ujrumani Joachi Loew |
Kocha wa Ujerumani Joachim Loew amesema kuwa timu
yake inapania kuandikisha historia kwa kuwa timu ya kwanza kutoka bara
Uropa kutwaa taji la dunia Kusini mwa Marekani usiku huu.
Ujerumani inakutana na Argentina katika fainali
ya kombe la dunia la mwaka huu huko Brazil baadaye usiku huu wa Jumapili tarehe 13
Julai katika uwanja wa kihistoria wa Maracana Ulioko mjini Rio de
Jenairo Brazil.
Hakuna timu yeyote kutoka barani Uropa ambayo
imewahi kushindwa taji la dunia katika michuano nane ya kombe la dunia
iliyoandaliwa Kusini mwa Marekani.
“Ninaamini kuwa kikosi changu kinauwezo wa kuandikisha rekodi ya dunia fauka ya matokeo ya zamani ya timu kutoka barani Uropa''
Hii itakuwa ni mara ya Tatu kwa timu hizo
kukutana katika fainali Ujerumani ikishinda mechi moja nayo Argentina
ikishinda ile nyengine(1986)
Argentina ilifuzu kwa fainali hizo baada ya
kuiondoa Uholanzi kupitia mikwaju ya penalti huku Ujerumani ikijikatia
tikiti yake ya Fainali baada ya kuifunza soka Brazil ilipoikomoa mabao
7-1 katika ile nusu fainali nyengine.
Licha ya hayo ,Loew amemlimbikizia sifa
kochokocho kocha mpinzani Alejandro Sabella akisema Argentina ameshinda
mechi zao zote licha ya ushindani mkali.
Maonni yake Loew yalitiliwa pondo na kiungo wake
wa kati Bastian Schweinsteiger aliyesema kuwa Ujerumani inauwezo wa
kuilaza Argentina licha ya wao kuonekana wakakamavu katika safu ya
ulinzi.
Hapa Messi , hapa Muller hatariiiiii |
Kocha Loew alikanusha dhana kuwa Argentina
imeumbwa kumnufaisha mshambulizi wa Barcelona Lionel Messi ,''La hasha
Argentina inawashambulizi wazuri hata wenye sifa sawa na Messi lakini
wao ndio wanaofanya kazi ya zida kisha messi anamaliza tu .
''Huwezi kuwapuuza washambulizi kama Gonzalo
Higuaín na Angel Di Maria, ukiwa unadhania Argentina ni Messi umekosea
sana''alisema kocha huyo.
No comments:
Post a Comment